Home Kaunti Maafisa wanasa sukari iliyokuwa ikiingizwa hapa nchini

Maafisa wanasa sukari iliyokuwa ikiingizwa hapa nchini

0
kra

Maafisa wa forodha katika kituo cha mpakani cha Malaba wamezuilia malori manne yaliyokuwa yamebeba sukari ya thamani ya mamilioni ya pesa.

Shehena hiyo ambayo ilinaswa Ijumaa saa kumi na moja asubuhi,  ilikuwa ikipelekwa mahali kusikojulikana nchini Kenya kutoka Uganda.

kra

Hata hivyo, afisa mkuu wa forodha ambaye alikataa kutajwa jina alisema ni lori mbili pekee ndizo zilizonaswa huku maafisa wa polisi wakithibitisha lori nne.

Afisa huyo aliwaelekeza wanahabari kwa mratibu wa shirika la ukusanyaji ushuru nchini-KRA eneo la Kisumu Patience Njau ambaye aliahidi kutoa taarifa siku ya Jumatatu.

Mwezi uliopita, basi la abiria lililokuwa likielekea Nairobi lilinaswa huko Bungoma na maafisa wa KRA kutoka Kisumu baada ya kuvuka hadi Kenya kupitia Malaba kutoka Kampala, ili kukwepa kituo cha ukaguzi cha mpakani cha Busia.

Lori hilo lilikuwa na shehena isiyojulikana ya bidhaa ambazo hazijadhibitiwa.

Baadhi ya wafanyikazi wa forodha na mawakala wa kuidhinisha bidhaa wameelezea wasiwasi kuhusu kupotea kwa mapato mengi kutokana na kukidhiri kwa visa vya kutoa hongo katika Kituo cha mpakani cha Malaba.

Wanadai kuwa mpaka wa Malaba umekuwa kitovu cha kupitisha bidhaa za magendo na kuendeleza biashara haramu ya binadamu.

Walimtaka waziri wa usalama wa taifa Prof Kithure Kindiki achukue hatua za haraka kukabiliana na tatizo hilo.

Website | + posts
Kennedy Epalat
+ posts