Home Habari Kuu Maafisa Wakuu wa polisi Kaunti ya Narok wahamishwa

Maafisa Wakuu wa polisi Kaunti ya Narok wahamishwa

Uhamisho wa maafisa hao unajiri baada ya mauaji ya soroveya wa umri wa miaka 29 Daniel Nkamasia.

0

Huduma ya taifa ya polisi imewahamisha maafisa wakuu wa polisi katika kaunti ya Narok.

Riko Ngare ndiye Kamanda mpya wa polisi katika kaunti ya Narok, akichukua mahala pa Kizito Mutoro, ambaye amehamishwa hadi kitengo cha polisi wa kusimamia shughuli za reli.

Mutoro, ambaye awali alihudumu wadhifa wa mlinzi wa rais mstaafu hayati Mwai Kibaki,  amehudumu katika kaunti ya Narok tangu mwaka 2019, alipotumwa kwa mara ya kwanza katika eneo hilo.

Mutoro atakumbukwa kwa wajibu muhimu aliotekeleza wa kuhakikisha usalama umeimarishwa katika kaunti hiyo, hususan katika eneo la Nkararo, kaunti ndogo ya Trans Mara Magharibi ambapo wakaazi walikuwa wakizozana kuhusu mipaka ya ardhi.

Vile vile Mutoro alifanikisha kuondolewa kwa watu waliokuwa wamevamia msitu wa Olokurto,, Sasimwani na ule wa Kirampa mwaka 2023.

Wakati huo huo afisa afisa mkuu wa kitengo cha polisi wa maswala ya jinai wa kaunti hiyo Mwenda Ethaiba, amehamishwa hadi kaunti ya Kericho katika wadhifa huo, akibadilishana na Peter Kieti.

Wengine waliohamishwa ni maafisa wote wa polisi katika vituo vya polisi vya Ololunga, Narosura, Narok Town, Nairegie Enkare, Suswa na Entasekerra.

Uhamisho wa maafisa hao unajiri baada ya mauaji ya soroveya wa umri wa miaka 29 Daniel Nkamasia.

Nkamasia aliuawa alipokuwa akifungua mlango kuingia nyumbani kwake, majuma mawili yaliyopita.

Website | + posts