Home Habari Kuu Maafisa wa zamani wa KDF watakiwa kufika katika Mahakama Kuu ya Mombasa

Maafisa wa zamani wa KDF watakiwa kufika katika Mahakama Kuu ya Mombasa

Maafisa hao wa jeshi la wanamaji waliachiliwa huru kwa makosa ya kususia kazi katika vikosi vya ulinzi nchini mwaka 2007 na mwaka 2008.

0

Afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma ODPP, imetoa agizo kwa maafisa wa zamani wa jeshi la wanamaji kujiwasilisha katika mahakama kuu ya Mombasa, ili kujitayarisha kusikizwa kwa rufaa zao, la sivyo watakamatwa tena, au rufaa hizo zitasikizwa bila wao kuwepo.

Kulingana na taarifa katika mtandao wa X, afisi hiyo ilisema mahakama ya kijeshi iliwapata maafisa hao na makosa ya kususia kazi.

Mahakama kuu ilifutilia mashtaka ya maafisa hao ya kususia kazi na badala yake kuwashtaki na makosa ya kutofika kazini bila ruhusa huku ikipunguza kifungo chao kutoka ile ya maisha hadi miaka miwili gerezani.

Maafisa hao wa jeshi la wanamaji waliachiliwa huru kwa makosa ya kususia kazi katika vikosi vya ulinzi nchini mwaka 2007 na mwaka 2008.

Maafisa hao wanadaiwa kuwa walienda kufanya kazi kwa kampuni za kiusalama za Marekani nchini Afghanistan, Iraq na Kuwait.

Walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama tatu za kijeshi katika kituo cha kijeshi cha Mtongwe.

Afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma inataka kesi hiyo isikizwe kwa haraka ili kuondolea mbali sintofahamu zinazozingira kesi hiyo, pamoja na kutoa mwongozo kwa mahakama za kijeshi kuhusu makosa ya kususia kazi.

Website | + posts