Home Habari Kuu Maafisa wa polisi wamkamata mshukiwa wa ugaidi

Maafisa wa polisi wamkamata mshukiwa wa ugaidi

Mnamo mwezi April 2023, washirika watatu wa mshukiwa huyo walikamatwa katika barabara kuu ya Isiolo- Moyale, walipojaribu kurejea hapa nchini.

0
Mshukiwa wa ugaidi Mustakima Mohammed Ali, akamatwa na polisi.

Maafisa wa polisi wa kukabiliana na ugaidi, wamemkamata mshukiwa wa ugaidi anayehusishwa na mauaji ya maafisa wawili wa polisi na chifu katika kaunti ya Lamu mwaka 2019.

Mustakima Mohammed Ali, alikamatwa Jumapili alasiri akiwa ndani ya basi iliyokuwa ikielekea Malindi katika operesheni iliyotekelezwa na maafisa wa kukabiliana na ugaidi wakisaidiwa na wale wa operesheni maalum katika kizuizi cha barabarani cha daraja la Sambaki.

Kulingana na idara ya upelelezi wa jinai DCI, baada ya Mustakima Ali almaarufu  Abu Mahir na washirika wake kutekeleza mauaji hayo, walijificha katika msitu wa Boni kabla ya kutorokea katika taifa moja jirani.

Mnamo mwezi April 2023, washirika watatu wa mshukiwa huyo walikamatwa katika barabara kuu ya Isiolo- Moyale, walipojaribu kurejea hapa nchini.

Walishatakiwa katika mahakama ya Kahawa, na kesi dhidi yao ingali inaendelea.

Kulingana na maafisa wa polisi, washukiwa wengine wa ugaidi ambao wametambuliwa, wanatafutwa.