Home Habari Kuu Maafisa wa polisi wakamatwa wakipokea hongo

Maafisa wa polisi wakamatwa wakipokea hongo

EACC imetoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za trafiki na kuripoti visa vyovyote vya kuitishwa hongo kupitia nambari ya EACC isiyotozwa malipo 1551.

0

Maafisa wanne wa polisi wa trafiki siku ya Jumanne walikamatwa wakipokea hongo katika barabara kuu ya Thika-Garissa.

Wanne hao Deborah Ngila Rosemary Nyokabi, Robert Kabiru na Christine Chebon, walifumaniwa na maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi, EACC wakipokea hongo.

“Kama sehemu ya kurejesha nidhamu katika polisi wa trafiki, EACC iliwakamata maafisa wanne wa trafiki wakipokea hongo kutoka kwa waendeshaji magari katika barabara kuu ya Thika-Garissa,” ilisema  EACC kupitia taarifa.

Katika kaunti ya Kisumu, tume hiyo ilimkamata Inspekta wa Polisi Joash Rotich wa kituo cha polisi cha Central kwa kuitisha hongo ya shilingi 500,000, ili aondoe mashtaka dhidi ya msafirishaji mmoja wa bidhaa.

EACC imetoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za trafiki na kuripoti visa vyovyote vya kuitishwa hongo kupitia nambari ya EACC isiyotozwa malipo 1551.

Website | + posts