Kizaazaa kilizuka katika barabara ya Naivasha- Mai Mahiu wakati maafisa wa tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi EACC, walipo wakamatwa maafisa wa polisi wa trafiki wakipokea hongo siku ya Alhamisi.
Mmoja wa maafisa hao wa trafiki alikataa kukamatwa na kufyetua risasi hewani huku akitoroka.
Akithibitisha kisa hicho afisa mkuu mtendaji wa tume ya EACC, Twalib Mbarak, alisema maafisa hao watafunguliwa mashtaka, huku waliotoroka watasakwa.
Twalib aliongeza kuwa anashauriana na Inspekta Jenerali wa polisi, Japheth Koome, kuhusu kutolewa kwa bunduki kwa polisi wa trafiki.
Maafisa hao watatu walipelekwa katika makao Makuu ya EACC katika jumba la Integrity na sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Milimani, wakisubiri kufikishwa mahakamani.