Home Kimataifa Maafisa wa mawasiliano serikalini wahimizwa kuwasilisha ipasavyo ajenda ya serikali

Maafisa wa mawasiliano serikalini wahimizwa kuwasilisha ipasavyo ajenda ya serikali

0
kra

Katibu katika Idara ya Utangazaji na Mawasiliano Prof. Edward Kisiang’ani amewahimiza maafisa wa mawasiliano katika idara mbalimbali za serikali kubuni mikakati mahsusi ya kuwasilisha ajenda ya serikali, kulingana na nguzo za mpango wa kuinua watu wa tabaka la chini kiuchumi almaarufu “Bottom-Up Economic Transformation – BETA”.

Nguzo kuu za mpango huo ni kilimo, biashara ndogo na za kadiri, makazi ya bei nafuu, huduma za afya kwa wote, maendeleo ya kidijitali na uchumi wa ubunifu.

kra

Akizungumza leo Jumatano kwenye mkutano wa siku tatu wa mafunzo kwa maafisa wa mawasiliano serikalini kuhusu mawasiliano ya serikali, jumbe na mahusiano na vyombo vya habari, ambao umeandaliwa na baraza la vyombo vya habari, MCK mjini Naivasha, katibu huyo alisema afisi za mawasiliano za serikali zinafaa kuangazia mahitaji ya wananchi.

Prof. Kisiang’ani alisema serikali inapanga kuimarisha haki ya umma kupata habari kwa kuhakikisha maafisa wa mawasiliano wanawezeshwa na wanapokea habari muhimu za serikali ambazo watawasilisha kwa wananchi.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Vyombo vya Habari David Omwoyo alisema kwamba maendeleo makubwa katika teknolojia yamebadilisha hali ya vyombo vya habari huku akihimiza maafisa wa mawasiliano serikalini kutumia fursa hiyo kuleta mabadiliko chanya.

Omwoyo alisema ni muhimu kwa maafisa wa mawasiliano serikalini kuwasiliana kila mara ili kuziba mianya ya mawasiliano.

Website | + posts