Home Habari Kuu Maafisa wa DCI wahimizwa kuimarisha doria kuhakikisha usalama

Maafisa wa DCI wahimizwa kuimarisha doria kuhakikisha usalama

Amin aliwahimiza maafisa hao waimarishe doria usalama, katika maeneo wanakohudumu, huku nchi hii ikijiandaa kwa msimu huo wa sherehe.

0
Mkurugenzi wa Idara ya DCI, Mohamed Amin.

Maafisa wa polisi wa idara ya upelelezi wa jinai, DCI wamehimizwa kuwa macho huku wananchi wanapojiandaa kwa msimu wa sherehe.

Mkurugenzi wa DCI Mohamed Amin amewaagiza wakuu wote katika makao makuu ya idara hiyo, makamanda wa kimaeneo na maafisa wa upepelezi wa jinai katika kaunti zote, waimarishe shughuli zao za kiusalama kabla ya msimu wa sikukuu.

Amin aliwahimiza maafisa hao waimarishe doria na usalama katika maeneo wanakohudumu, huku nchi hii ikijiandaa kwa msimu wa sherehe.

Aliongeza kuwa ni wakati wa msimu kama huu ambapo wahalifu huamua kuvuruga amani na usalama wa wananchi kupitia wizi wa kimabavu na uhalifu wa kila aina.

Aliwaagiza makamanda wote kufanya kila juhudi kuhakikisha usalama upo nyakati zote ili Wakenya waendelee na shughuli zao za kila siku za kiucumi na sherehe miongoni mwao.

Aliyasema hayo Ijumaa wakati wa mkutano ulioandaliwa kabla ya sherehe za mwisho wa mwaka za idara ya DCI katika makao makuu ya idara hiyo jijini Nairobi.

Website | + posts