Home Michezo Lyles na Jackson wahifadhi mataji ya mita 200 mashindano ya Riadha ulimwenguni

Lyles na Jackson wahifadhi mataji ya mita 200 mashindano ya Riadha ulimwenguni

0
BUDAPEST, HUNGARY - AUGUST 25: Sha'Carri Richardson of Team United States, Gabrielle Thomas of Team United States, Shericka Jackson of Team Jamaica and Marie-Josee Ta Lou of Team Ivory Coast react after the Women's 200m Final during day seven of the World Athletics Championships Budapest 2023 at National Athletics Centre on August 25, 2023 in Budapest, Hungary. (Photo by Christian Petersen/Getty Images for World Athletics)

Shericka Jackson wa Jamaica  na Noah  Lyles wa Marekani wamedhihirisha umaahiri  wao baada ya kuhifadhi mataji ya dunia ya mita 200 katika siku ya saba ya mashindano yanayoendelea mjini Budapest,Hungary  Ijumaa usiku.

Noah Lyles wa Marekani akishinda fainali ya mita 200  (Photo by Christian Petersen/Getty Images for World Athletics)

Jackson akiyekuwa ameshinda  fedha katika mita 100 mwaka huu akikamilisha fainali hiyo akiweka rekodi mpya ya mashindano ya sekunde 21 nukta 41, akifuatwa na  Gabrielle Thomas wa Marekani kwa sekunde 21 nukta 81 , huku Sha Carri Richardson wa Marekani pia  akinyakua nishani ya shaba kwa sekunde 21 nukta 91.

BUDAPEST, HUNGARY – : Shericka Jackson wa  Jamaica akishinda mbio za mita  200  (Photo by Stephen Pond/Getty Images for World Athletics)

Lyles alihifadhi taji ya wanaume akiziparakasa kwa sekunde 19 nukta 52,akifuatwa na mwenzake Erriyon Khighton kwa sekunde 19 nukta  75, huku Letsile Tebogo wa Botswana akiridhia nishani ya shaba kwa sekunde 19 nukta 81.