Chama cha Wanasheria nchini (LSK) kimewasilisha kesi ya dharura mahakamani kupinga utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2023 ikisema kuwa ni kinyume cha sheria na katiba ya Kenya.
LSK inasema kuwa utekelezaji wa sheri hiyo mpya utakuwa mzigo zaidi kwa Wakenya ambao tayari wanataabika kutokana na gharama ya juu ya maisha.
Kesi hii inawasilishwa wiki moja baada ya makahama ya rufaa kuondoa agizo lililokuwa limeweka na mahakama kuu kuzuia utekelezaji wa sheria hiyo.
Wafanyakazi wote wataanza kukatwa mishahara kuanzia mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu kulipia matozo ya nyumba ya asilimia 1.5.