Home Habari Kuu LSK yalalamika kuhangaishwa na maafisa wa usalama

LSK yalalamika kuhangaishwa na maafisa wa usalama

0

Chama cha Wanasheria Nchini, LSK kimelaklamikia kile kinachodai kuwa kutishwa kwa baadhi ya wanachama wake.

Rais wa chama hicho Eric Theuri amedai kuwa maafisa wa kitengo cha upelelezi, DCI na wale wa vitengo vingine vya kiusalama wamekuwa wakijaribu kufungua mashtaka ya uhalifu dhidi ya mawakili wanapotekeleza majukumu yao.

Chama hicho sasa kimeitaka serikali kuwahakikishia mawakili mazingira bora ya utendaji kazi ili kuwahudumia wateja wao bila kuingiliwa.

Chama hicho pia kimetoa wito kwa afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma kutetea maslahi ya umma.

Matamshi hayo yanajiri baada ya jaribio la kampuni moja inayohusishwa na afisa mmoja mkuu wa umma la kutaka wakili mmoja na mfanyabiashara mmoja jijini Nairobi kufunguliwa mashtaka ya ulaghai kutibuka.

Hayo ni baada ya Hakimu Mkuu wa mahakama ya Milimani Lucas Onyina kusitisha mashtaka ya uhalifu dhidi ya wakili Moses Abongo Owour na Ohas Otieno, ambaye  ni mkurugenzi wa kampuni ya Columbus 2000.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here