Klabu ya Police FC imemteua kocha wa Croatia Zdravko Logarusic, kuwa kocha mpya kutwaa nafasi ya Francis Baraza, aliyetimuliwa kufuatia msururu wa matokeo mabovu.
Baraza amefurushwa Police FC akiiacha katika nafasi ya 16 ligini ikiwa na alama tatu pekee kutokana na michuano minne .
Logarusic amezinduliwa Alhamisi na mwenyekiti wa Nyale Munga na atakuwa akiifunza timu ya tatu katika ligi kuu ya Kenya, baada ya awali kuzifunza Gor Mahia na AFC Leopards.
Mtihani wa kwanza kwa Logarusic utakuwa mechi ya ugenini Jumamosi hii dhidi ya Bidco United