Home Michezo Liverpool yainyuka Newcastle na kupanua uongozi wa EPL

Liverpool yainyuka Newcastle na kupanua uongozi wa EPL

0

Timu ya Liverpool ilipanua uongozi wa ligi kuu ya Uingereza, EPL kwa alama tatu baada ya kuishinda Newcaste United magoli 4-2 katika mechi ya kusisimua iliyogaragazwa katika uwanja wa Anfield jana Jumatatu usiku. 

Magoli mawili yaliyofungwa na Mohamed Salah huku Curtis Jones na Cody Gapko wakifunga goli moja kila mmoja yaliwahakikishia vijana wa Jürgen Klopp ushindi dhidi ya Newcastle United iliyojituma mchezoni.

Magoli ya Newcastle United yalitiwa kimiani na wachezaji Alexander Isak na Sven Botman.

Liverpool sasa inaongoza jedwali la ligi kuu kwa alama 45 huku ikifuatwa Aston Villa iliyo na alama 42 na Manchester City walio na alama 40 wakiwa hawajacheza mechi moja ikilinganishwa na mechi 20 zilizochezwa na timu zingine.

Arsenal iliyocharazwa na West Ham magoli 2-1 siku chache zilizopita ni ya nne ligini kwa alama 40.