Home Michezo Lionel Messi moto wa kuotea mbali

Lionel Messi moto wa kuotea mbali

Messi mwenye umri wa miaka 35 amefunga magoli matano na kusaidia moja katika mechi tatu pekee za Inter Miami ya David Beckham

0
Lionel Messi moto wa kuotea mbali: Picha kwa hisani

Maisha ya soka ya mchezaji bora duniani Lionel Messi yanazidi kuwa matamu zaidi nchini Marekani huku nyota huyo wa timu ya taifa ya Argentina akiendeleza msururu wa kuvunja rekodi moja baada ya nyingine.

Jambo la kushangaza, imemchukua michuano mitatu tu kuingia kwenye chati za wafungaji 10 bora wa muda wote wa klabu ya Inter Miami.

Messi mwenye umri wa miaka 35 amefunga magoli matano na kusaidia moja katika mechi tatu pekee za Inter Miami ya David Beckham, rekodi tosha ya kumjumuisha miongoni mwa mabingwa wa klabu hiyo ambayo imekuwa hai kutoka mwaka wa 2020.

Japo klabu ya Inter Miami ni klabu mpya, imeshiriki ligi ya MLS miaka mitatu sasa na kwa mchezaji Lionel Messi ambaye ni bingwa wa Kombe la Dunia kufunga mabao matano ndani ya jumla ya dakika 203 ni jambo la kihistoria klabuni hapo.

Hawa hapa ni wafungaji bora wa klabu ya Inter Miami ya Marekani.

Mchezaji mwenza wa Zamani wa Argentina Gonzalo Higuain anaongoza orodha hii baada ya kufungia klabu hiyo mara 29 kati ya mwaka 2020-2022. Leonardo Campana ambaye bado anaichezea Inter Miami ni wa pili na mabao 16, idadi ambayo Lionel Messi anaweza akaifukuzia ifikiapo mwishoni mwa msimu.

 

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here