Home Michezo Lionel Messi ashinda tuzo ya Ballon d’Or

Lionel Messi ashinda tuzo ya Ballon d’Or

Mshambulizi wa timu ya Ufaransa Kylian Mbappe, alitajwa wa tatu katika tuzo hiyo.

0
Mshambulizi wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi.

Mshambulizi wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Inter Miami Lionel Messi, ameshinda kwa mara ya nane tuzo ya wanaume ya Ballon d’Or.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, alitambuliwa katika hafla iliyoandaliwa Jijini Paris Ufaransa, kwa kuisaidia nchi yake kushinda kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana.

Messi sasa amezidisha ushindi wa Ballon d’Or dhidi ya mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland.

“Ni furaha kufika hapa tena, kusherehekea hafla hii. Kufanikiwa kushinda kombe la dunia, na kuafikia ndoto yangu” alisema Messi.

Kiungo wa kati wa Uingereza na Real Madrid, Jude Bellingham alishinda tuzo la Kopa la mchezaji bora dunia mwenye umri wa chini ya miaka 21, katika hafla hiyo.

Mshambulizi wa timu ya Ufaransa Kylian Mbappe, alitajwa wa tatu katika tuzo hiyo.

Website | + posts