Linturi ‘mweupe kama pamba’ baada kukwepa meno ya mamba

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa Kilimo Mithika linturi.

Waziri wa Kilimo Mithika Linturi amenusurika kutimuliwa afisini na kamati ya wabunge 11, baada ya kuondolewa mashtaka yote katika sakata ya mbolea ghushi.

Kwenye ripoti iliyowasilishwa  bungeni kwenye kikao maalum siku ya Jumatatu na mwenyekiti wa kamati hiyo Naomi Waqo,Waziri hakuwa na hatia .

Wabunge 6 wa kamati hiyo maalum walipiga kura kumwokoa Linturi, huku wanne wakipiga kura ya kutaka atimuliwe afisini kwa utepetevu.

Kulingana na ripoti hiyo,mwasilishi wa hoja ya kumbandua afisini Linturi ambaye ni mbunge wa Bumula Jack Wamboka, alishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya Waziri kwenye sakata hiyo.

Wabunge 149 walipiga kura ya kumtimua Waziri Linturi, huku 36 wakimtetea kwenye kura iliyopigwa wiki iliyopita bungeni.

Website |  + posts
Share This Article