Home Biashara Linda Wambani ateuliwa kaimu katibu wa kampuni ya Safaricom

Linda Wambani ateuliwa kaimu katibu wa kampuni ya Safaricom

0

Linda Mesa Wambani ameteuliwa kaimu katibu mpya wa kampuni ya mawasiliano   ya Safaricom .

Uteuzi huo unafuatia kujiuzulu kwa Kathryne Maundu, aliyekuwa amehudumu kwa kipindi cha miaka saba.

Kulingana na taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Safaricom Adil Khawaja ,Wambani ataanza rasmi majukumu yake Oktoba mosi.

Wambani ni wakili aliye na tajriba ya zaidi ya miaka 19,na pia ana shahada ya uanasheria kutoka chuo kikuu cha Nairobi kando na shahada ya masuala ya usimamizi kutoka chuo kikuu cha kimatifa cha Marekani USIU na shahada ya uzamifu kuhusu uanasheria wa mahakama ya viwandani kutoka chuo kikuu cha Nairobi .

Website | + posts