Home Michezo Ligi ya Mabingwa Afrika kurejea Jumanne

Ligi ya Mabingwa Afrika kurejea Jumanne

0

Kipute cha kuwania kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika kitaingia mechi za raundi ya nne hatua ya makundi siku ya Jumanne  Disemba 19 na Jumatano Disemba 20.

Kundi A ,Mamelodi Sundowns wanaongoza kwa alama sawa na TP Mazembe,Nouadhibou na Pyramids FC kila timu ikiwa na pointi 4, baada ya kushinda mchuano mmoja na kwenda sare moja baada ya mechi tatu.

Pyramids watawaalika Sundowns Jumanne,wakati Mazembe wakiwa nyumbani dhidi ya Nouadhubou ya Mauritania.

Asec Mimosas wanaongoza kundi B kwa alama 7,wakifuatwa na Jwaneng Galxy kwa pointi 4, huku Wydad na Simba SC zikiwa na pointi 3 na 2 mtawalia.

Simba watakuwa nyumbani kwa Mkapa dhidi ya Wydad Casablanca katika mchuano ambao wenyeji hawana budi kushinda, ili kuweka hai matumaini ya kuingia robo fainali, wakati Jwaneng wakiwa ziarani Ivory Coast dhidi ya Mimosas.

Petro Atletico ya Angola wanaongoza kundi C kwa alama 7 ,wakifuatwa na Esperance walio na pointi 4, huku Etoile Du Sahel na Al Hilal Omdurman kutoka Sudan zikiwa na alama 3 kila moja.

Petro itakuwa nyumbani Luanda kupambana na Esperance huku Al Hilal wakiwatumbuiza Sahel.

Mabingwa watetezi Al Ahly wanaoshiriki nusu fainali ya Kombe la Dunia wanaongoza kundi A kwa alama 5, wakifuatwa na Medeama na CR Belouizdad kwa alama 3 kila moja huku Yanga wakiburura mkia kwa pointi 2.

Yanga watakuwa nyumbani kwa Mkapa katika mechi pekee ya kundi hilo dhidi ya Medeama.