Home Michezo Ligi kuu ya mabingwa ulaya kurejelewa leo.

Ligi kuu ya mabingwa ulaya kurejelewa leo.

Awamu ya pili ya raundi ya 16 bora ya ligi kuu ya mabingwa ulaya, itaanza Leo. Washindi mara sita wa taji hilo Bayern Munchen wa ujerumani watakaribisha Lazio wa italia.

Katika raundi ya kwanza, Lazio waliwalaza Bayern kwa bao moja, jambo lililowagadhabisha washika dau wa mamba hao wa ujerumani na hata kusababisha kuanzishwa kwa mipango ya kuteua kocha mwingine.

Katika mchuano wa leo, lazima Bayern washinde kwa mabao mengi ili kufuzu kwa awamu ya nane bora.

Mchuano mwingine wa leo ni baina ya Real Sociedad ya Uhispania na PSG ya Ufaransa. Kule Ufaransa wenyeji walivuna ushindi wa magoli mawili kwa sufuri.

Leo hii, itakuwa fursa ya Real Sociedad kujikwamua mbele ya mashabiki wa nyumbani ingawa utakuwa mtihani mgumu kwa sababu ya kiu ya muda mrefu waliyonayo PSG.

Michuano hili miwili itaanza sa tano usiku.

Kesho mabingwa mara 14 Real Madrid wa Uhispania, watawakaribisha RB Leipzig. Real waliwalaza Leipzig bao moja kule Ujerumani na hivyo ushindi au sare ya aina yeyote hapo kesho, itawavusha hadi raundi ya nane bora.

Vile vile, kesho tutashuhudia mabingwa watetezi Man City wakipepeta dhidi Copenhagen. kwenye awamu ya kwanza , Man City walimiliki mchezo na kushinda kwa Mabao matatu kwa Moja.

Michuano mingine itachezwa juma lijalo.

Website | + posts
Boniface Musotsi
+ posts