Home Michezo Leverkusen kukabiliana na Atalanta fainali ya kombe la Europa League

Leverkusen kukabiliana na Atalanta fainali ya kombe la Europa League

0

Mabingwa wa Ujermani Bayer Leverkusen watakabiliana na Atalanta ya Italia katika fainali ya kuwania kombe la Europa League, Jumatano usiku mjini Dublin katika Jamhuri ya Ireland.

Atalanta wanawania kutawazwa mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe hilo, huku Leverkusen wakilenga taji ya pili na ya kwanza  tangu mwaka 1988.

Uga wa Dublin Arena utakaoandaa fainali ya kombe la Europa League

Leverkusen wanajivunia rekodi ya kutoshindwa katika mechi 52 msimu huu na watashuka ugani Dublin wakiazimia kudumisha rekodi yao.

Katika robo fainali Leverkusen  waliibandua Westham United ya Uingereza mabao  3-1,kabla ya kuwatema AS Roma ya Italia magoli 4-2 katika semi fainali.

Upande wao Atalanta wanajivunia kutopoteza mechi katika michuano 12 iliyopita, na waliibandua Liverpool magoli 3-1 katika robi fainali, kabla ya kuicharaza  Olympic Marseille ya Ufaransa mabao 4-1 katika nusu  fainali.

Mechi ya Jumatano usiku itakuwa ya tatu baina ya timu hizo mbili ambapo Atalanta waliishinda Leverkusen 3-2 katika mkumbo wa kwanza wa raundi ya 16 bora, kabla ya kuwagutusha Wajerumani nyumbani walipowafyatua goli moja bila jibu katika mechi ya marudio.

Website | + posts