Lamu kunadiwa kama kisiwa cha tamasha

Martin Mwanje
1 Min Read

Tamasha ya kitamaduni ya mwaka 2023 ilimalizika kwa mbwembwe za aina yake mwishoni mwa wiki iliyopita huku Bodi ya Utalii Nchini, KTB ikitangaza mipango ya kuinadi upya Lamu kama kisiwa cha tamasha ili kuwavutia watalii wengi kisiwani hapo. 

Washiriki wapatao 30,000 wakiwemo watalii wa kigeni kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uholanzi, Poland, Italia na Asia walishiriki tamasha hiyo ya siku tatu.

Mashindano ya punda na soka ya ufukweni ni miongoni mwa vitu vilivyonadiwa wakati wa tamasha hiyo.

Akiwahutubia wadau wa utalii pembezoni mwa tamasha hiyo, mwenyekiti wa KTB Francis Gichaba alisema tamasha kadhaa zilizoandaliwa kisiwani hapo mwaka huu zina uwezo wa kuendelea kuwavutia watalii katika kisiwa cha Lamu.

“Kando na tamasha ya kitamaduni ya Lamu ambayo imekinadi kisiwa hicho kote duniani, pia tuna tamasha za  Maulid, Yoga, tamasha za chakula, sanaa na tamasha za uvuvi za Lamu miongoni mwa zingine ambazo zinaendelea kuwavutia watalii na washiriki wengine kwa eneo hilo. Hii ndio sababu pamoja na wadau wa utalii wa Lamu, tunafanya mipango ya kuhamasisha tamasha hizi mwaka wote,” alisema Gichaba.

Website |  + posts
Share This Article