Home Habari Kuu Kuria asema usajili wa NYS utakuwa huru na wazi

Kuria asema usajili wa NYS utakuwa huru na wazi

0

Waziri wa utumishi wa umma na utendakazi Moses Kuria, amekariri kuwa zoezi la uteuzi wa watakaojiunga na huduma ya taifa kwa vijana NYS litakuwa huru na wazi.

Kuria amesma zoezi hilo linalotarajiwa kuanza hivi karibuni halitakuwa na mapendeleo kwa yeyote.

Awali mwaka uliopita waziri Kuria alidokeza kuwa vijana wa NYS watapewa kipa umbele katika usajili wa makurutu wanaojiunga na vikosi vya jeshi,polisi na huduma ya magereza.

Usajili wa watakaojiunga na huduma yabkitaifa kwa vijana utaandaliwa baina ya Februari 5 na 9 mwaka huu kote nchini.

Vijana 15,000 wanatarajiwa kuteuliwa katika zoezi la usajili la mwezi ujao.

Website | + posts