Home Habari Kuu KUPPET yatishia kususia mitihani ya kitaifa

KUPPET yatishia kususia mitihani ya kitaifa

0

Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo, KUPPET kimetishia kususia mtihani wa kitaifa wa KCSE na mitihani ya vyuo ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Uongozi wa KUPPET unalalamikia malipo duni ya usimamizi na usahihishaji wa mtihani wa kidato cha nne, KCSE.

Chama hicho kinataka kuongezwa kwa malipo na kuboreshwa kwa mazingira ya kufanya kazi kwa wasimamizi na wasahihishaji wa mitihani hiyo kabla ya kutoa huduma zao.

Endapo KUPPET watatekeleza tishio lao, mtihani wa KCSE utaathirika kwa kiwango kikubwa.

Website | + posts