Home Habari Kuu KUPPET yatilia shaka uporaji wa shilingi bilioni 115 za hazina ya uzeeni

KUPPET yatilia shaka uporaji wa shilingi bilioni 115 za hazina ya uzeeni

0

Chama cha walimu wa shule za sekondari na vyuo  nchini KUPPET kimenahofia uporaji wa shilingi bilioni 115 za hazina ya uzeeni maarufu kama Public Service Superannuation Scheme (PSSS),kufuatia kucheleweshwa uteuzi wa wanachama wa bodi .

Kulingana na KUPPET hawana imani na usalama wa pesa za wanachama wao kwani PSSS haijakuwa na maafisa wa bodi tangu Disemba mwaka 2023.

PSSS ni hazina ya pili kwa ukubwa nchini Kenya baada ya NSSF ikiwa na wanachama 420,000 huku 360,000 wakiwa walimu wanaochangisha shilingi bilioni 3.6 kila mwezi.

Website | + posts