Home Habari Kuu Kundi moja la wapiganaji ladai kuwateka nyara wanajeshi wa Israel

Kundi moja la wapiganaji ladai kuwateka nyara wanajeshi wa Israel

Islamic Jihad ni mojawapo ya makundi kadhaa ya wapiganaji wanaoendesha harakati zao huko Gaza.

0
Israel ilishambuliwa na wanamgambo wa Hamas, Jumamosi asubuhi.
kra

Kundi la Jihad la Kiislamu (Islamic Jihad) ambalo linaendesha harakati zake Gaza, linadai wapiganaji wake pia wamewakamata wanajeshi kadhaa wa Israeli, Msemaji wake Abu Hamza alisema kwenye chapisho la Telegram,

“Tunathibitisha katika Brigedi za al-Quds kwamba sasa, shukrani kwa Mwenyezi Mungu, tunamiliki askari wengi wa Kizayuni ambao ni wafungwa mikononi mwetu.”

kra

Islamic Jihad ni mojawapo ya makundi kadhaa ya wapiganaji wanaoendesha harakati zao huko Gaza.

Brigedi ya Quds ni tawi lake la silaha. Kundi hilo linashirikiana na Hamas lakini pia linadumisha uhuru.

Pia linafanya kazi katika Ukingo wa Magharibi na limefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Waisraeli.

Hayo yanajiri wakati ambapo waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amewaambia raia wa nchi hiyo kuwa wako vitani baada ya taifa hilo kushambuliwa na wanamgambo wa Hamas.

“Raia wa Israeli. Tuko vitani, sio operesheni, sio kuongezeka kwa vita.

“Leo asubuhi Hamas ilitekeleza shambulio la kushtukiza la mauaji dhidi ya taifa la Israel na raia wake. Tumekuwa nalo tangu mapema asubuhi,” alisema Netanyahu.

Website | + posts
BBC
+ posts