Home Habari Kuu Kundi la M23 ladai kutwaa eneo la Rubaya nchini DRC

Kundi la M23 ladai kutwaa eneo la Rubaya nchini DRC

0

Kundi la waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo limedai kutwaa eneo la Rubaya, lenye madini mengi ya Coltan yanayotumika kutengeneza simu za rununu.

Haya ni kwa mjibu wa msemaji wa kundi la M23 Willy Ngoma,  aliyeongeza kuwa wametwaa eneo hilo kufuatia makabiliano makali na wanajeshi kauli ambayo haijathibitishwa na msemaji wa jeshi Luteni Kanali Guillaume Njike.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters Njike ,alisema hawawezi kubainisha iwapo M23 wametwaa eneo hilo jinsi wanavyodai au la.

Maeneo mengi yanayochimbwa madini yanapatiakna mashariki mwak Congo na yamekumbwa na vita na mizozo ya mara kwa mara, huku kundi la M23 lithibiti ngome hiyo tangu mwaka 2022

Website | + posts