Home Biashara KTB: Sekta ya kibinafsi muhimu kwa ukuaji utalii nchini

KTB: Sekta ya kibinafsi muhimu kwa ukuaji utalii nchini

0

Bodi ya Utalii Nchini, KTB imehusisha kunawiri kwa biashara ya utalii nchini na ushirikiano thabiti uliopo kati ya serikali na sekta ya kibinafsi. 

Kulingana na KTB, ushirikiano huo hususan katika kuwapeleka watalii kujionea vivutio muhimu na kuhudhuria makongamano ya kibiashara umesaidia mno kupunguza matumizi ya moja kwa moja ya serikali kufuatia matatizo ya kifedha.

Hayo ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa bodi hiyo Francis Gichaba aliyezungumza wakati wa Programu ya kwanza ya Tuzo za Magical Kenya Loyalty iliyofanyika pembezoni mwa toleo la tatu la Maonyesho ya Usafiri wa Kanda ya Afrika Mashariki, EARTE.

“KTB iko tayari kufanya kazi na washikadau wote kuhakikisha tunaonyesha thamani kwa wanaoweza kuwa wasafiri. Lengo letu ni kufikia watalii milioni  5.5 katika kipindi cha miaka mitano ijayo, na kila mtu ana jukumu la kutekeleza katika hili,” alisema Gichaba.

“Hii ndio kwa sababu tuna mipango ya Tuzo za Magical Kenya Loyalty, ambayo ni muhimu katika kutambua wajibu unaofanywa na washikadau wa utalii na washirika wetu katika kuhakikisha ukuaji wa biashara ya utalii.”

Website | + posts