Home Taifa KQ yafafanua kuhusu kufungwa kwa njia ya ndege uwanjani JKIA mapema leo

KQ yafafanua kuhusu kufungwa kwa njia ya ndege uwanjani JKIA mapema leo

0
Ndege ya shirika la Kenya Airways.

Kampuni ya uchukuzi wa ndege nchini Kenya Airways KQ imefafanua kuhusu kisa cha kutua kwa ndge iliyokuwa na hitilafu kilichosababisha kufungwa kwa mojawapo ya njia za ndege katika uwanja wa JKIA.

kupitia taarifa usimamizi wa KQ umeelezea kwamba ulipokea taarifa kutoka kwa usimamizi wa uwanja wa ndege wa Sharjah huko UAE kuhusu kupatikana kwa mabaki ya kile kinachoaminika kuwa mabaki ya gurudumu la ndege ya KQ iliyokuwa ikitoka UAE kuelekea Juba.

KQ ilibadili mkondo wa ndege hiyo na badala ya kuelekea Juba ikaelekezwa Nairobi kwa ajili ya kuangaliwa na walipochunguza wakapata ni kweli gurudumu moja lilikuwa na hitilafu lakini halingeathiri kutua kwa ndege hiyo.

Hata hivyo wakati wa kutua, gurudumu jingine likapata hitilafu na ndege hiyo ikakwama kwenye njia moja katika uwanja wa JKIA na kusababisha kufungwa kwa njia hiyo ya ndege.

Kampuni hiyo na mamlaka ya kusimamia viwanja vya ndege nchini KAA zilishirikiana kubadilisha magurudumu ya ndege hiyo na baadaye ikaondolewa kwenye njia hiyo ya ndege kunako saa nane na dakika 12 mchana wa leo.

Usimamizi wa KQ umeomba radhi kwa yeyote aliyeathirika na hatua ya kufungwa kwa njia hiyo ya ndege na kuhakikishia umma kwamba kila kitu sasa kiko shwari katika uwanja wa ndege wa JKIA.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here