Home Vipindi KPA yashutumiwa kwa kutozingatia sheria ya jinsia ya thuluthi mbili

KPA yashutumiwa kwa kutozingatia sheria ya jinsia ya thuluthi mbili

kra

Halmashauri ya bandari nchini, KPA haijazingatia sheria ya jinsia ya thuluthi mbili katika uajiri wa wafanyakazi wake kulingana na ripoti ya kamati ya bunge kuhusu mshikamano wa kitaifa na usawa wa kijinsia.

Kulingana na ripoti hiyo, halmashauri hiyo ina wafanyakazi 1,433 pekee wa kike kati ya wafanyakazi 6,522, idadi hiyo ikiwa ni asilimia 22 pekee.

kra

Mkurugenzi Mkuu wa halmashauri hiyo William Ruto amesema hatua hiyo inatokana na mazingira ya kikazi kwenye halmashauri hiyo ambayo hutegemea mashine, mitambo pamoja na kazi za uhandisi.

Wanachama wa kamati hiyo pia walihoji kwa nini ni watu wa jamii chache pekee walioajiriwa kwenye halmashauri hiyo.

Akijibu hayo, Ruto alisema wafanyakazi wengi ni wa jamii zinazopakana na bandari ya Mombasa.

Website | + posts
feedback@kbc.co.ke | Website | + posts