Home Michezo KPA watwaa taji FIBA Afrika mashariki baada ya kuwazidia nguvu wenyeji REG...

KPA watwaa taji FIBA Afrika mashariki baada ya kuwazidia nguvu wenyeji REG ya Rwanda

0

Kenya Ports Authority walitawazwa mabingwa wa ligi ya wanawake ya FIBA katika mpira wa kikapu baada ya kwuazidia maarifa wenyeji Rwanda Energy Group alama 87-53 kwenye fainali iliyopigwa Jumamosi katika ukumbi wa Lyncee mjini Kigali, Rwanda.

KPA walishinda robo ya kwanza 22-16 na kutwaa ya pili pointi 22-14 wakiongoza alama 44-30 kufikia mapumzikoni.

Vipusa wa Kenya alinyakuab robo yatatu alama 18-13 na kutwaa ya mwisho 25-10.