Cybrian Kotut wa kenya amemaliza wa pili kwenye makala ya 50 ya mbio za Berlin Marathon zilizoandaliwa mapema Jumapili mjini Berlin Ujerumani.
Kotut alitumia muda wa saa 2 dakika 3bna sekunde 22 kuzikamilisha ,nyuma ya Milkesa Mengesha wa Ethiopia aliyetwaa ubingwa kwa saa 2 dakika 3 na sekunde 17.
Alew, Haymanot pia kutoka Ethiopia alichukua nafasi ya tatu kwa saa 2 dakika 3 na sekunde 31 huku Stehen Kiprono akiambulia nafasi ya nne.
Tigist Ketema wa Uhabeshi aliwaongoza wenzake kufagia nafasi nne za kwanza katika shindano la wanawake akikata utepe kwa sa 2 dakika 16 na sekunde 42 ,sekunde 12 mbele ya Fikir, Mestawot aliyemaliza wa pili, huku Mulatie, Bosena akichukua nafasi ya tatu kwa kutumia saa 2 na dakika 19 .