Home Habari Kuu Koskei: Hakuna atakayesazwa katika vita dhidi ya ufisadi

Koskei: Hakuna atakayesazwa katika vita dhidi ya ufisadi

Koskei aliuhimiza mfumo wa haki usitumiwe kuwakinga wahalifu.

0

Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, amesema kuwa vita dhidi ya ufisadi vitaimarishwa.

Koskei aliyekuwa akihutubu kwenye warsha ya wanahabari kuhusu uhalifu na uongozi iliyoandaliwa jijini Mombasa, alisema hakuna yeyote atakayesazwa na kwamba serikali itatekeleza vita hivyo kuambatana na sheria inapowachukulia hatua wale wanaoshukiwa kufuja rasilmali za umma.

Kama sehemu ya kuimarisha vita dhidi ya ufisadi mkuu wa utumishi wa umma alisema kuwa serikali inatafakari kuratibu sheria itakayowezesha tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi, (EACC) kusalia na sehemu fulani ya fedha zinazotokana na uhalifu ili kutimiza nakisi ya bajeti yake.

Koskei aliuhimiza mfumo wa haki usitumiwe kuwakinga wahalifu.

Kwa upande wake afisa mkuu wa tume ya EACC, Twalib Mbarak, aliyehudhuria warsha hiyo alisema kuwa tume hiyo hupokea zaidi ya kesi 9,000 za ufisadi na imefanikiwa kurejesha shilingi bilioni- 23.74 kuanzia mwaka 2018 hadi 2023.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa tume hiyo inaweza kutekeleza shughuli zake kwa njia bora zaidi iwapo itapewa rasilmali zaidi kwani shilingi bilioni 3.4 inazotengewa kwa mwaka hutumika hasa kulipa mishahara huku asilimia 34 ikisalia kutekeleza shughuli zake.

Website | + posts