Home Kimataifa Korti yatoa kibali cha kukamatwa kwa Gavana wa Uasin Gishu

Korti yatoa kibali cha kukamatwa kwa Gavana wa Uasin Gishu

0
Jonathan Bii, Gavana wa Uasin Gishu
kra

Mahakama ya Nakuru leo Jumatatu imetoa kibali cha kukamatwa kwa Gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii na aliyekuwa Naibu Gavana wa kaunti hiyo John Barorot. 

Barorot alijiuzulu wadhifa huo siku chache zilizopita baada ya kupata kazi nyingine ya kimataifa.

kra

Kibali hicho kilitolewa baada ya wawili hao kukosa kufika mahakamani kutoa ushuhuda kuhusiana na sakata ya ufadhili wa masomo nchini Finland.

Sakata hiyo ilisababisha wazazi wengi kupoteza mamilioni ya pesa huku wanao wakikosa kwenda Finland kusoma jinsi waliovyahidiwa.

Wazazi hao mara kwa mara wameandamana mjini Eldoret wakishinikiza kukamatwa kwa wahusika katika kashfa hiyo akiwemo aliyekuwa Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago na watu wengine wawili.

Mandago ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka yanayofungamana na sakata hiyo anahudumu kama Seneta wa kaunti ya Uasin Gishu.

 

 

Website | + posts