Home Habari Kuu Korti yasema KICC ni mali ya serikali

Korti yasema KICC ni mali ya serikali

0
DP_RUTO MALINDII

Jumba la Mikutano ya Kimataifa la Kenyatta, KICC ni mali ya serikali. 

Hii ni kwa mujibu wa uamuzi uliotolewa leo Jumatatu na Jaji Jacqueline Mogeni wa Mahakama Kuu.

Awali, chama cha KANU kiliwasilisha kesi mahakamani kikidai kuwa mmiliki halali wa jumba hilo.

Hata hivyo, Jaji Mogeni ametangua hatimiliki iliyokabidhiwa chama hicho miongo mitatu iliyopita na kuitaja Wizara ya Utalii kuwa mmiliki halali wa ardhi ilikojengwa KICC.

Hali ya vuta ni kuvute imeshamiri tangu chama cha KANU kuwasilisha kesi mahakamani mnamo mwaka wa 2003 kikidai kumiliki ardhi palipojenjwa KICC pamoja na jengo hilo.

Ilidhaniwa kuwa uamuzi wa mahakama wa leo Jumatatu ungesitisha kivumbi cha kisheria ambacho kimedumu kwa miongo kadhaa, lakini chama hicho kimesema kitakata rufaa dhidi ya uamuz huo.

Kupitia Mkurugenzi wake wa Mawasiliano Manasse Nyainda, chama cha KANU kimesikitikia uamuzi wa mahakama na kuashiria kuwa kimewaelekeza wanasheria wake kukata rufaa.

“Chama cha KANU kimesikitikia mno uamuzi uliotolewa na leo Nairobi na Jaji Jacqueline Mugo wa Mahakama Kuu kuhusiana na utata wa umiliki wa kipande cha ardhi palipojengwa jumba la KICC,” alisema Nyainda katika taarifa.

“Chama tayari kimetoa maelekezo kwa timu yake ya wanasheria kuwasilisha ilani ya rufaa mara moja wakati chama kikitathmini hukumu hiyo ili kitoe taarifa ya kina badaye.”

 

 

Website | + posts