Home Kimataifa Koome afafanua kuhusu kutwaliwa kwa maiti ya Kennedy Onyango

Koome afafanua kuhusu kutwaliwa kwa maiti ya Kennedy Onyango

0
kra

Inspekta jenerali wa polisi Japhet Koome amefafanua kuhusu kutwaliwa kwa maiti ya mtoto aliyefariki baada ya kupigwa risasi nane huko Rongai wakati wa maandamano.

Kupitia taarifa, Koome alisema kwamba hatua hiyo ya kutwaa maiti ya mtoto Kennedy Onyango inatokana na juhudi za jamaa aliyetambuliwa kuwa babake mzazi.

kra

Mama ya mtoto huyo na watu wake wa karibu akiwemo mwanaharakati na mchekeshaji Eric Omondi walikuwa kwenye safari kuelekea Mbita kaunti ya Homa Bay jana Jumamosi wakati walikitana na polisi ambao walikagua gari lililokuwa limebeba maiti na kuchukua mwili wa marehemu.

Kisa hicho kilizua minong’ono kwenye mitandao ya kijamii pale ambapo video ya mama Kennedy ilipochaposhwa ikimwonyesha akilia kwa uchungu.

Anasikika akitoa ombi kwa yeyote aliyesababisha kutwaliwa kwa mwili wa mwanawe aurejeshe uzikwe ili apate faraja moyoni.

Omondi naye alitoa ombi sawia kwenye again zake za mitandao ya kijamii akisema mama huyo ameteseka sana na aliyetoa amri ya kutwaa maiti ya mtoto huyo amhurumie na amkubalie azike mwanawe.

Koome alikanusha ripoti kwamba huduma ya taifa ya polisi ndiyo inahusika na kutwaliwa kwa maiti hiyo akielezea kwamba agizo lilitolewa na mahakama ya Mbita na polisi wa eneo hilo hawakuwa na budi ila kulitekeleza.

Mahakama hiyo iliamuru mwili huo usizikwe bali uhifadhiwe katika makafani ya hospitali ya kaunti ndogo ya Suba kutoa fursa ya kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi.

Website | + posts