Home Habari Kuu Kongamano la usafi wa mazingira na utawala kufanyika Kisumu

Kongamano la usafi wa mazingira na utawala kufanyika Kisumu

0
kiico

Zaidi ya washiriki 5,000 wakijumuisha washikadau kutoka idara ya maji na usafi wa mazingira ya humu nchini na kote duniani, wanatarajiwa kuhudhuria kongamano la maji, usafi wa mazingira na utawala mjini Kisumu mwezi juni.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na muungano wa kusambaza maji na usafi kwa ushirikiano na wizara ya maji na unyunyuziaji mashamba maji, serikali ya kaunti ya Kisumu na kampuni ya maji na usafi ya Kisumu-KIWASCO, litajadili mikakati ya kutimiza malengo ya kuwepo Kwa maji safi na changamoto zinazokumba usambazaji wake kwa watu wengi na kudumisha usafi kote nchini.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa muungano wa wanaotoa huduma za maji WASPA, Antony Ombugo, washikadau kama vile wawakilishi wa serikali za kaunti na ile ya kitaiifa wamethibitisha kwamba watahudhuria.

Kongamano hili linajiri wakati nchi ya Kenya imeonekana kwenda mwendo wa kobe katika kutimiza malengo 6 ya maendeleo ya kudumu (SDG) kwani ni asilimia 60 ya wakenya wanapata maji safi huku swala la usafi wa mazingira likisalia mtihani mkuu hasa ikitiliwa maanani kuwa ni watu millioni 3.9 pekee nchini wanatumia mfumo wa maji taka.

kiico