Home Kimataifa Kongamano la ugatuzi kuzinduliwa rasmi kesho

Kongamano la ugatuzi kuzinduliwa rasmi kesho

0
kra

Rais William Ruto kesho Jumatano atazindua rasmi awamu ya 8 ya kongamano la ugatuzi ambalo linaandaliwa katika gatuzi la Uasin Gishu, mjini Eldoret.

Ruto tayari amefika kwenye gatuzi hilo ambapo amekuwa akifanyia kazi ikulu ndogo ya Eldoret. Jana Jumanne, alihudhuria kwa njia ya mtandao mkutano kuhusu mabadiliko katika sekta ya mifugo katika maeneo kame.

kra

Aliandaa pia mkutano na viongozi kadhaa wa eneo hilo wakiwemo maafisa wa utawala kama vile makamishna ambapo aliwaonya dhidi ya kukubalia uhalifu wa aina yoyote katika maeneo yao na iwapo hilo litatokea, kila mmoja wao atawajibika kibinafsi.

Kaulimbiu ya kongamano hilo linaloandaliwa kati ya tarehe 15 na 19 mwezi huu ni: Miaka 10 ya Ugatuzi: Yanayojiri Sasa na Yajayo.

Viongozi kadhaa wamepangiwa kuhutubia kongamano hilo akiwemo kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye atazungumza siku ya Alhamisi.

Naibu Rais Rigathi Gachagua atafunga rasmi kongamano hilo siku ya Ijumaa.

Website | + posts