Home Kimataifa Kongamano la Afrika kuhusu Tabia Nchi ni la kipekee, asema Rais Ruto

Kongamano la Afrika kuhusu Tabia Nchi ni la kipekee, asema Rais Ruto

0
kra

Kongamano la Afrika kuhusu Tabia Nchi lililoanza leo Jumatatu jijini Nairobi na ambalo ni la kwanza kuwahi kufanyika ni la kipekee.

Kongamano hilo linalowaleta pamoja wajumbe wapatao 30,000 kutoka kote duniani lilifunguliwa rasmi na Rais William Ruto katika jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta, KICC.

kra

Rais Ruto anasema kuna haja ya kuwa na shabaha inayoangazia fursa zilizopo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuhakikisha uthabiti na ustawi wa bara la Afrika.

“Kuhakikisha maendeleo na afya nzuri ya idadi inayoongezeka ya watu barani Afrika bila kuifanya dunia kukabiliwa na janga kubwa zaidi si kitu cha nadharia, ni kitu halisi kinachowezekana kilichothibitishwa na sayansi na tajiriba inayochipuka. Shabaha inayoangazia fursa zilizopo za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ndio nguzo ya kuichochea Afrika kufikia uthabiti na ustawi, ikituinua hadi kiwango cha uchumi wa kati na kuzidi hapo,” alisema Rais Ruto wakati akizindua kongamano hilo.

“Muktadha huu ndio hasa unaolifanya Kongamano hili la Tabia Nchi kutofautiana na mengine. Linalenga kutuunganisha  sote kama majirani, sekta, taasisi, mabara na vizazi vyote. Ni kwa sababu sote tuna maslahi katika uwezo wa dunia kuhakikisha uhai wetu, kwa kuwa na maono ya mustakabali unaokumbatia maadili ya usawa, usalama wa binadamu na ustawi wa pamoja.”

Rais Ruto akitumia fursa hiyo kuwaambia wajumbe kuwa Afrika ina vigezo vyote vinavyohitajika kufikia mustakabali huo.

“Mali yetu kuu ni vijana na nguvukazi inayoongezeka, iliyoelimika, yenye ujuzi na motisha ya kukuza viwanda, ubunifu na ujasiriamali.”

Website | + posts