Home Michezo Kocha Firat ataja kikosi cha Harambee Stars

Kocha Firat ataja kikosi cha Harambee Stars

0
kra

Kocha wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars Engine Firat ametaja kikosi kitakachosafiri Jumatatu Septemba 2, kuelekea Uganda kwa mechi ya kwanza ya kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao dhidi ya Zimbabwe.

Kikosi kilichotangazwa kinawajumuisha Makipa Levis Opiyo, Patrick Matasi na  Byrne Omondi.

kra

Mabeki ni pamoja na Sharrif Majabe, Joseph Okumu, Johnstone Omurwa, Amos Nondi, Abud Omar, Eric Ouma, Sylvester Owino na Alphonce Omija.

Wachezaji wa kiungo ni pamoja na Chris Erambo, Richard Odada, Anthony Akumu, Kenneth Muguna, Eric Johanna, Ronney Onyango, Austine Odhiambo, Duke Abuya na Timothy Ouma

Washambulizi ni John Avire, Michael Olunga, Jonah Ayunga, Benson Omalla na  Victor Omune.

Kenya itamenyana na Zimbabwe katika mechi ya kwanza ya kundi J, kufuzu kwa kipute cha AFCON Septemba 6, kabla ya kusafiri Jumamosi ijayo  kwenda Afrika Kusini kwa pambano la pili Septemba 10, dhidi ya The Brave Warriors ya Namibia.

Timu nyingine katika kundi J pamoja na Kenya ni Cameroon.

Mechi za kufuzu kwa fainali za AFCON zitakamilika mwezi Novemba mwaka huu

 

Website | + posts