Home Michezo Kocha Firat aelezea sababu ya Harambee Stars kuchezea mechi za nyumbani nchini...

Kocha Firat aelezea sababu ya Harambee Stars kuchezea mechi za nyumbani nchini Malawi

0

Kocha wa timu ya taifa Harambee stars Engin Firat, amesema wamelazimika kuchezea mechi za nyumbani nchini Malawi baada ya Kenya kukosa viwanja vinavyoafiki viwango vilivyowekwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Kwa mujibu wa kocha huyo, Stars wanaufahamu fika uga wa Kitaifa wa Bingu baada ya kunyakua taji la mechi za mataifa manne mwezi machi dhidi ya The Flames ya Malawi na The Warriors ya Zimbabwe.

Firat aliyasema haya katika uwanja waPolice Sacco wakati wa matayarisho kwa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2026 , tarehe saba na 11 mwezi ujao dhidi ya Burundi na Côte d’Ivoire mtawalia.

Kocha huyo hata hivyo alisisitiza umuhimu wa kuwa na viwanja vya nyumbani ambavyo huwapa mashabiki nafasi kubwa ya kujitokeza na kushabikia timu yao ikilinganishwa kuchezea taifa la kigeni.

Kikosi cha Harambee Stars kinachowajuisha wachezaji 25 kitaondoka nchini Juni 2 huku wengine wanaocheza nje ya nchi kama mshambulizi Micheal Olunga, Daniel Anyembe na Richard Odada wakijiunga nao baadaye.

Beki Eric Ouma a.k.a Marcelo pia huenda akajiunga kwani hatima ya jeraha lake haijulikani.

Mataifa mengine kwenye kundi hilo ni Gambia, Gabon na Seychelles.

Kenya ilishindwa na Gabon magoli mawili Kwa Moja na kuirindima Ushelisheli mabao matano Kwa sufuri katika mechi za ufunguzi za kundi F kufuzu kwa kombe la dunia mwaka uliopita.