Home Kimataifa KNUT yataka mshahara wa walimu kuongezwa kwa asilimia 60

KNUT yataka mshahara wa walimu kuongezwa kwa asilimia 60

KNUT pia kupitia kwa katibu mkuu wake Nelson Oyuu, imekuwa ikitaka kuchunguzwa upya kwa mwafaka wa Pamoja wa maelewano kuhusu mishahara ya walimu wa mwaka 2021 na 2025

0
kra

Chama cha Kitaifa cha Walimu Nchini, KNUT kimependekeza nyongeza ya asilimia 60 kwa mshahara wa walimu kote nchini.

Mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Patrick Karinga amesema kuwa walimu wana mzigo mkubwa wa kuwahudumia wanafunzi nchini huku majukumu yao yakitarajiwa kuongezeka mwaka ujao wakati elimu ya mtaala wa umilisi, CBC itakapoingia gredi ya nane mwaka ujao.

kra

KNUT pia kupitia kwa Katibu Mkuu wake Nelson Oyuu imekuwa ikitaka kuchunguzwa upya kwa Mwafaka wa Pamoja wa Maelewano (CBA) kuhusu mishahara ya walimu wa mwaka 2021-2025.

Chama hicho kimetoa makataa ya siku saba kwa Tume ya Kuwaajiri Walimu, TSC kuitisha kikao kuhusu pendekezo hilo.

Website | + posts