Home Kimataifa KMTC yatangaza nafasi za mafunzo katika vyuo vyake 83

KMTC yatangaza nafasi za mafunzo katika vyuo vyake 83

Tarehe ya mwisho kutuma maombi ni Agosti 4 .

0

Chuo cha mafunzo ya matibabu nchini KMTC kimetangaza kufungua kupokea maombi kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuanza masomo mwezi Septemba mwaka huu.

Kulingana na arifa iliyoandikwa na afisa mkuu mtendani Dkt Agnes Wahome,wanafunzi wanaotimiza alama zinazohitajika wanatakiwa kutuma maombi kupitia kwa Portal ya KUCCPS https://students.kuccps.net.

wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne KCSE kutoka mwaka 2013 hadi 2022 wanahitaji kutuma maombi kwa kuchagua moja kati ya kozi 30 zinazopatikana katika tuvuti ya KUCCPS huku waatakaofaulu wakiitwa kujiunga na vyuo 83 vya KMTC kote nchini.

Kozi hizo zinzjumuisha zile za stahada na Certificate katika masomo ya community health nursing, mental health and psychiatry, midwifery, radiography and imaging, medical laboratory sciences, occupational therapy, optometry, pharmacy, physiotherapy and public health, miongoni mwa mengine.

Tarehe ya mwisho kutuma maombi ni Agosti 4 .

Bi Wahome pia amefafanua kuwa siku ya mwisho kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya mafunzo ya walimu wa shule za msingi wameongezewa muda hadi Agosti 4.

Website | + posts