Home Habari Kuu Kituo cha mabasi cha Green Park kubadilishwa na kujengwa jumba la mikutano

Kituo cha mabasi cha Green Park kubadilishwa na kujengwa jumba la mikutano

0

Kituo cha mabasi cha Green park jijini  Nairobi sasa kitabadilishwa na kuwa kituo cha kuandaa mikutano.

Gavana wa jiji la Nairobi Johnson Sakaja amesema mradi huo uliotekelezwa na iliyokuwa mamlaka ya jiji la Nairobi NMS kwa kitita cha shilingi milioni 180 ulikosa kuafikia lengo lake.

Isitoshe, mwanakandarasi aliyetekeleza mradi huo anadai shilingi milioni 90 miaka miwili baada ya kuukamilisha.

Lengo kuu la mradi huo lilikuwa kupunguza msongamano wa magari kati kati ya jiji, lengo hilo likisalia kitendawili.

“Kituo hicho cha Green Park ambacho ni cha ekari tano, kiko mahali muhimu zaidi katikati ya jiji. Hakikupaswa kuwa kituo cha mabasi,” alisema Gavana Sakaja.

Alidokeza kuwa mipango inatekekezww kujenga jumba la mikutano sawia na jumba la mikutano la Kigali, ambalo litawavutia wawekezaji wengi na kuongeza mapato ya taifa.

Kituo cha Green Park pia kina sehemu za biashara kama vile maduka, hoteli na kituo cha polisi.

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here