Home Habari Kuu Kituo cha Banya Fort chafunguliwa kuunganisha Kenya na Ethiopia

Kituo cha Banya Fort chafunguliwa kuunganisha Kenya na Ethiopia

0
Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Raymond Omollo.

Serikali imewataka Wakenya wanaoishi mpakani Marsabit kushirikiana na vyombo vya dola kuimarisha usalama kutokana na kudorora kwa hali ya usalama katika upembe wa Afrika.

Katibu katika Wizara ya Usalama wa Kitaifa Dkt. Raymond Omollo amesisitiza kuwa jamii ina jukumu kubwa kulinda usalama.

Dkt. Omollo aliyasema hayo jana Alhamisi alipoongoza ufunguzi wa mpaka wa Banya Fort, ambao ndio eneo jipya la kuingia na kutoka nchini Kenya ukiunganisha Kenya na Ethiopia.

Alisisitiza kuwa jamii za eneo hilo zipo katika nafasi nzuri ya kutambua shughuli na watu wa kutilia shaka kati yao na kufanya ushirikiano wao kuwa muhimu katika kukabiliana na matishio ya usalama.

“Ni kupitia kushirikishana taarifa za kijasusi na taarifa husika ndiposa tunaweza kuwatambua na kukabiliana na wahalifu ambao ni tishio kwa ustawi wetu wa pamoja na maendeleo makubwa yaliyotabiriwa kwa wakazi na serikali ya kaunti ya Marsabit na taifa kwa jumla,” alisema Dkt. Omollo.

 

 

Website | + posts