Home Michezo Kisumu kuandaa mechi za AFCON 2027, asema Rais Ruto

Kisumu kuandaa mechi za AFCON 2027, asema Rais Ruto

0

Kaunti ya Kisumu itaandaa baadhi ya mechi za kipute cha kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027 maarufu kama AFCON.

Hakikisho hilo limetolewa siku ya Jumatatu na Rais William Ruto alipozindua meli ya MV Uhuru 2.

Rais amesisitiza kuwa michuano ya AFCON ya mwaka 2027 humu nchini itaandaliwa katika kaunti mbalimbali na kuondoa hofu kuwa mechi hizo zingechezwa katika kaunti za Nairobi na Uasin Gishu pekee.

Kenya imeratibiwa kuandaa kipute hicho kwa pamoja na mataifa jirani ya Tanzania na Uganda.

Ruto amesema mashindano yoyote ya soka ya Afrika Mashariki au ya Afrika yatakuwa yakiandaliwa katika kaunti kadhaa nchini na wala sio kaunti moja au mbili pekee.

Gavana Anyang’ Nyongo wa Kisumu na mwenzake wa Kakamega Fernandes Barasa, awali walilamikia hatua ya mechi hizo kuandaliwa katika miji ya Nairobi na Eldoret pekee.

Website | + posts