Home Kimataifa Kisa cha nne cha Mpox charipotiwa nchini Kenya

Kisa cha nne cha Mpox charipotiwa nchini Kenya

0
kra

Katibu wa afya ya umma Mary Muthoni ametangaza kuwa Kenya imeripoti kisa cha nne cha ugonjwa wa Mpox .

Kulingana na Muthoni kisa chja hivi punde kinamshirikisha mwendeshaji lori aliyekuwa akitoka Mombasa kuelekea nchini Rwanda.

kra

Kulingana na taarifa ya Bi Muthoni kupitia mtandao wake wa X mwathiriwa alijihisi kuwa na mgogoro wa afya mnamo Agosti 28, akipitia Gilgil na kusitisha safari yake.

Mafisa wa afya ya dharura katika kaunti ndogo ya Gilgil walifika mahali hapo na kumpeleka katika kituo cha wagonjwa wanaotengwa ambapo amelazwa ingawa hayumo hatarini.

Visa vingine vya awali vimeripotiwa katika kaunti za Taita Taveta, Busia na Nairobi.

Watu 30 wanaoaminika kutangamana na mgonjwa huyo katika kaunti za Busia,Mombasa,Nairobi na Nakuru pia wanatafutwa ili kufanyiwa uchungizi .

Kulingana na taarifa ya Wizara ya afya watu wapatao 599,380 wamechunguzwa dhidi ya ugonjwa huo kufikiwa Agosti 31 wakiwemo 16,533 katika maeneo ya mipakani.

Website | + posts