Home Habari za Hivi Punde Kipyegon,Chebet na Chelimo watua fainali ya mita 5,000 Olimpiki

Kipyegon,Chebet na Chelimo watua fainali ya mita 5,000 Olimpiki

0
kra

Bingwa wa dunia katika mita 5,000 Faith Kipyegon amewaongoza wenzake Margaret Chelimo na Beatrice Chebet, kufuzu kwa fainali ya mbio hizo  baada ya kutamba katika mchujo wa  Ijumaa.

Kipyegon ambaye ni bingwa mara mbili wa Olimpiki katika mita 1500 amedhibiti mchujo wa kwanza na kuongoza kwa dakika 14 sekunde 57.56, akifuatwa na bingwa mtetezi Sifan Hassan wa Uholanzi.

kra

Margaret Chelimo Kipkemboi wa kenya pia amejikatia tiketi kwa fainali ya Jumatatu usiku baada ya kumaliza wa nne kwa dakika 14 sekunde 57.70.

Chebet ambaye ni mshikilizi wa rekodi ya  dunia ya mita 10,000  ameongoza mchujo wa pili akizikamilisha kwa dakika 15 nukta 73.

Fainali ya shindano hilo itaandaliwa Jumatatu usiku.

Website | + posts