Home Michezo Kipyegon na Chepkoech kufunga msimu Eugene Jumamosi

Kipyegon na Chepkoech kufunga msimu Eugene Jumamosi

Kipyegon ambaye ni bingwa mara mbili wa Olimpiki ameshinda mikondo mitatu ya Doha,Florence na Monaco na atahifadhi taji ya  mwaka jana endapo ataibuka mshindi.

0
Faith Kipyegon

Bingwa mara tatu wa dunia katika mbio za mita 1,500 Faith Kipyegon na mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji  Beatrice Chepkoech watajitosa uwanjani jumamosi usiku, katika mkondo wa 14 na wa mwisho wa mashindano ya Diamond League mjini Eugene Mareakani.

Kipyegon ambaye ni bingwa mara mbili wa Olimpiki ameshinda mikondo mitatu ya Doha,Florence na Monaco na atahifadhi taji ya  mwaka jana endapo ataibuka mshindi.

Chepkeoch atapambana kwa mara ya tatu mtawalia na bingwa wa dunia Winfred Yavi wa Bahrain mzawa wa Kenya katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji na atakayeshiriki huku pia atakayeshinda akitawazwa mshindi wa msimu.

Wakenya wengine kwenye fainali hiyo ni bingwa wa jumuiya ya madola Jackline Chepkoech na mshindi wa nishani ya shaba ya dunia mwaka huu Faith Cherotich.

Upande wa wanaume mshindi wa nishani ya shaba ya dunia katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji Abraham Kibiwott, atawaongoza wenzake Benjamin Kigen,Simon Kiprop na Amos Serem wakitoana jasho na bingwa wa dunia Sofiane El Bakkali wa Morocco.

Mkondo huo wa 14 utakamilika Jumamosi usiku huku washindi wa kila fani katika fani zote 32, wakituzwa almasi kitita cha pesa na tiketi ya kushiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao jijini Paris Ufaransa.

Website | + posts