Home Michezo Kipyegon kuwinda rekodi ya tatu Monaco Diamond League

Kipyegon kuwinda rekodi ya tatu Monaco Diamond League

Kipyegon anajivunia muda bora wa dakika sekunde 16 nukta 71 alioandikisha mwaka 2015.

0

Mshikilizi wa rekodi mbili za dunia Faith Kipyegon atashuka uwanjani Ijumaa usiku, Julai 21 akiwa na lengo moja la kuwinda rekodi ya tatu atakaposhiriki mkondo wa Monaco Diamond League nchini Ufaransa.

Kipyegon ambaye ni bingwa mara mbili wa dunia na Olimpiki atashiriki mbio za umbali wa maili moja akijaribu kuvunja rekodi yake Sifan Hassan wa Uholanzi ya dakika 4 sekunde 12 nukta 33 aliyoandikisha mwaka 2019.

Kipyegon anajivunia muda bora wa dakika sekunde 16 nukta 71 aliouandikisha mwaka 2015.

Bingwa wa Jumuiya ya Madola Ferdinand Omanyala atajitosa katika mbio za mita 100 akiwania ushindi wa kwanza wa Diamond League.

Omanyala ambaye pia ni bingwa wa Afrika atalazimika kukabiliana na Akani Simbine wa Afrika Kusini, Letsile Tebogo wa Botswana na Yohan Blake wa Jamaica.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here