Home Kimataifa Kipyegon kuwania dhahabu Olimpiki

Kipyegon kuwania dhahabu Olimpiki

0
kra

Faith Kipyegon atawania kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda dhahabu tatu mtawalia katika fainali ya mita 1,500, atakapojitosa uwanjani  Jumamosi usiku kwenye fainali ya shindano hilo.

Kipyegon ambaye alishinda dhahabu ya Olimpiki mwaka  2016 na  na kuhifadhi mwaka  2021,  anawinda dhahabu hiyo, baada ya kukosa  dhahabu  ya fainali ya  mita 5,000.

kra

Bingwa huyo wa dunia atashiriki fainali hiyo pamoja na mwanariadha wa Kenya mwenye makao yake  nchini Marekani  Susan Ejore.

Fainali hiyo itaanza saa tatu na robo.